IQNA

Pepo Katika Qur'ani /10

Baraka za Pepo Kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu

18:03 - February 14, 2024
Habari ID: 3478352
IQNA – Baraka za pepo kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu ni za aina mbalimbali, zingine ni za kimaada (material), zingine ni za kiroho, na zingine ni kutokuwepo kwa shida na usumbufu.

Katika Surah Al-Fatir, Aya ya 33, Qur'ani inarejea kwenye nyenzo: “Mabustani ya milele watayaingia. Huko watavikwa vikuku vya dhahabu, na lulu, na nguo zao humo ni za hariri."

Waumini waliopuuza matamanio ya dunia na hawakutafuta kuvaa nguo za kifahari duniani watapata nguo na vito bora kabisa huko akhera.

Asili ya baraka za peponi haieleweki kikamilifu kwa wale wanaoishi katika ulimwengu huu. Kwa mfano, ingawa baadhi ya maelezo kuhusu mavazi ya watu wa peponi yanafanana na yale ya hapa duniani, kwa hakika yanatofautiana kimaumbile. Maelezo haya yamekusudiwa kuonyesha jinsi mavazi ya peponi yalivyo mazuri, ya kuvutia na ya kustarehesha.

Katika aya inayofuata, amani ya akili na kutokuwepo kwa huzuni kunatajwa kama baraka ya kiroho ya paradiso:

Na watasema: Alhamdulillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye tuondolea huzuni zote. Hakika Mola wetu Mlezi bila ya shaka ni Mwenye kusamehe, Mwenye shukrani.” (Aya ya 34 ya Surah Al-Fatir).

Sifa mbili za Mwenyezi Mungu zilizotajwa mwishoni mwa Aya, nazo ni Ghafour (Mwenye kusamehe) na Shakour (Mzidishishaji wa thawabu) zinaonyesha kuwa baraka za peponi ni matokeo ya Mwenyezi Mungu kusamehe na kwamba Mwenyezi Mungu huzidisha malipo ya matendo mema.

Katika aya inayofuata, tunasoma: “(Wale wanaoingia peponi husema:) Ambaye kwa fadhila yake ametuweka makao ya kukaa daima; humu haitugusi taabu wala humu hakutugusi kuchoka. (Aya ya 35 ya Surah Al-Fatir)

Kwa hiyo katika paradiso au pepo, kila kitu kinachohitajiwa ili kupata amani ya akili na furaha kinapatikana. Katika ulimwengu huu, watu wengine wanaweza kuwa na ustawi na mali lakini utulivu na amani ya akili ni nadra. Watu wa peponi, hata hivyo, sio tu kuwa na ustawi na faraja, lakini pia wako mbali na huzuni na masaibu yoyote. Peponi ni mahali penye amani ya kweli na hakuna huzuni, mateso na taabu.

3487155

Kishikizo: qiyama
captcha