IQNA

Pepo Katika Qur'ani /9

Majina na Ngazi za Pepo katika Quran

17:19 - February 13, 2024
Habari ID: 3478347
IQNA – Qur’ani Tukufu inaitaja pepo kwa majina na sifa mbalimbali, ambazo baadhi yake zinatilia mkazo sifa maalumu ya pepo na baadhi nyingine zinaashiria pepo maalumu zilizoandaliwa kwa ajili ya waumini kulingana na safu zao.

Jannat al-Naeem, Jannat al-Adn, Jannat al-Firdaus, Jannat al-Khuld, Jannat al-Maawa, Dar as-Salaam, Dar al-Muqama, na Dar al-Qarar ni miongoni mwa majina ya pepo yaliyotajwa katika Qur'ani Tukufu.

Baadhi ya majina haya, kama vile Dar as-Salaam, ambayo ina maana ya nyumba ya amani na afya, labda hutumiwa kurejelea sehemu moja ya pepop. Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 127 ya Surat Al-Anaam:

"Hao watapata na Dar as-Salaam (nyumba ya amani) kwa Mola wao Mlezi."

Katika Surah Al-Fatir, pepo inajulikana kwa mara ya kwanza kama Jannat al-Adn kisha inanukuu watu wa peponi wakiitaja Dar al-Muqama.

Baadhi ya majina ya peopo, hata hivyo, labda yanaelekeza kwenye safu na viwango tofauti. Qur'ani Tukufu inataja sehemu ambayo baadhi ya watu wa peponi wataishi kama Jannat al-Adn, wengine kama Jannat al-Maawa, kundi jingine kama Jannat al-Firdaus na jingine kama Jannat al-Naeem.

Kwa mujibu wa Hadith, Mtukufu Mtume (SAW) amesema: “Peponi kuna ngazi mia moja, kilicho baina ya kila ngazi mbili ni kama kilicho baina ya mbingu na ardhi. Al-Firdaus ndio daraja la juu kabisa, na kutoka humo mito minne ya peponi inatiririshwa. Basi unapomuomba Allah SWT, muombeni Jannah Al-Firdaus.”

Hii ina maana kwamba kila mtu, haijalishi hadhi yake juu ya njia ya ukamilifu ni ya juu kiasi gani, hatakiwi kuridhika na nafasi hiyo bali ajitahidi kuhamia kwenye hadhi na kiwango cha juu kwa kuongeza elimu yake, kufanya matendo mema zaidi na Tahdhīb al-Nafs   yaani kuitakasa na kuiboresha.

Kwa wazi, kadiri kiwango cha imani, matendo, elimu na maadili ya mtu kilivyo juu, ndivyo baraka za kimungu zinavyoongezeka zaidi katika akhera. Quran Tukufu inasema katika Aya ya 132 ya Surah Al-Anaam:

"Na wote wana daraja mbali mbali kutokana na yale waliyo yatenda. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na yale wanayo yatenda."

Daraja na viwango katika ulimwengu huu ni rahisi au  sahili lakini viwango na vyeo vya watu waadilifu katika suala la imani, matendo mema na ukaribu na Mungu vina nukta kadhaa muhimu.. Kwa mfano, mtu anaweza kuwa na daraja la juu kutokana na kupata kifo cha kishahidi lakini mtu mwingine anaweza kuwa juu zaidi yake kwa vyeo kwa sababu ya unyenyekevu wake.

 Qur'ani Tukufu inasema katika Aya ya 21 ya Surah Al-Isra:

“Angalia vipi tulivyo wafadhili baadhi yao kuliko wenginewe. Na hakika Akhera ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi".

3487133

Kishikizo: qiyama
captcha