IQNA – Kisomo cha Qur’ani Tukufu kwa tarteel kilichorekodiwa na wanafunzi wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri kitaanza kurushwa hewani kupitia Idhaa ya Qur’ani ya Cairo kuanzia leo.
IQNA – Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi Arabia siku ya Jumapili imezindua rasmi Mkutano na Maonesho ya 5 ya Hajj kwa mwaka 1447 Hijria, yanayoendelea kuanzia tarehe 9 hadi 12 Novemba 2025 katika jiji la Jeddah, chini ya kauli mbiu “Kutoka Makkah Hadi Ulimwenguni.”
IQNA – Awamu ya kwanza ya mashindano ya Qur’ani Tukufu ya Sheikh Jassim bin Muhammad bin Thani imeanza rasmi nchini Qatar, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Awqaf na Mambo ya Kiislamu.
IQNA – Mradi wa kutafsiri Qur'an kwa lugha ya Rohingya umeanzishwa katika mazingira ambapo Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakilengwa na dhulma na kufukuzwa kutoka ardhi yao kwa miongo kadhaa. Lengo lake ni kuziba pengo la maarifa ya Kiislamu na kupambana na ukandamizaji wa lugha ya Rohingya.
IQNA – Washairi kutoka nchi 25 wamewasilisha takriban mashairi 1,500 katika Tamasha la Kimataifa la Ushairi la “Mtume wa Rehema,” lilioandaliwa kwa heshima ya kutimia miaka 1500 tangu kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW).
IQNA – Katika kura ya maamuzi yenye uzito, Shirikisho la Soka la Ireland (FAI) limeunga mkono azimio linaloitaka UEFA kuifukuza Israel kutoka kwenye mashindano ya kimataifa na ya vilabu barani Ulaya.
IQNA – Kituo cha Uchapishaji na Usambazaji wa Qur'an Tukufu cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimeanza kutumia teknolojia za Akili Mnemba (AI) kwa ajili ya kutengeneza nakala za Qur'ani za kidijitali, hatua inayofungua ukurasa mpya wa kuunganisha urithi wa kiroho na ubunifu wa kisasa.
IQNA – Takriban walowezi haramu 3,939 Waisraeli waliuvamia msikiti mtukufu wa Al-Aqsa wiki iliyopita wakiwa chini ya ulinzi wa majeshi ya utawala wa Kizayuni, kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni.
IQNA – Qur’ani Tukufu inakataza waziwazi aina yoyote ya ushirikiano katika maovu au uonevu. Katika Surah Al-Ma’idah aya ya 2, Allah anasema: “Wala msisaidiane katika dhambi na uadui.”
IQNA – Mashambulio dhidi ya misikiti nchini Uingereza yameripotiwa kuongezeka kwa kasi katika miezi ya hivi karibuni, huku ripoti mpya ikihusisha ongezeko hilo na harakati za utaifa zinazotumia alama za Kikristo na za Uingereza katika vitendo vya vitisho.
IQNA – Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri kimelaani mlipuko wa bomu uliotokea katika msikiti mjini Jakarta, mji mkuu wa Indonesia, wakati wa Sala ya Ijumaa, na kujeruhi watu kadhaa.
IQNA – Katika mandhari ya vijijini vya Malawi, taswira za watoto wakishiriki kwa ari katika miduara ya kisomo cha Qur'ani Tukufu zimeanza kuvutia mitandaoni, zikidhihirisha mchango hai wa jamii ya Waislamu wachache nchini humo.
IQNA – Mtaalamu wa afya ya akili nchini Iran ameonya kwamba matumizi kupita kiasi ya mitandao ya kijamii yanawafanya vijana kujitenga, huku yakibadilisha maadili yao. Ameitaka jamii ya wazazi Waislamu kuamiliana na watoto kwa huruma, subira na mfano wa vitendo, si kwa kuwabana na kuwadhibiti.
IQNA-Operesheni ya pamoja ya kukabiliana na ugaidi kati ya Jamhuri ya Ireland na Ireland Kaskazini imefanikiwa kuzuia shambulio lililopangwa dhidi ya msikiti na vituo vya wahamiaji, na kupelekea kunaswa vilipuzi na kufikishwa mahakamani kwa wanaume wawili ambao sasa wanakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na tukio hilo.
IQNA-Katika ripoti mpya iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya Uswidi, imebainika kuwa idadi kubwa ya wanafunzi Waislamu wamekuwa wakihama shule kutokana na kukumbwa na ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu.